Kwa Nini Whitemark? - Whitemark Hotels

Go to content

Main menu:

Kwa Nini Whitemark?

UTAIPATA UBUNGO: Whitemark Hotel ipo karibu kabisa na Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani iliyopo Ubungo, Vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Ardhi , Millenium Business Park , Benjamini Mkapa Special Economic Zone na Mlimani City na makutano ya barabara za Nelson Mandela na Morogoro.  

Ni rahisi kufika Whitemark Hotel kwa basi au taxi kutoka katikati ya mji (Posta na Kariakoo), Bandari ya Dar es Salaam na uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere.

Vilevile Hotel ipo katikati ya Hotel nyingine nyingi, lodge na nyumba za kulaza wageni, hii inatoa fursa kwa makundi ya watu kuweza kulala kwa ukaribu huku kila mmoja akichagua mahali pa kulala kulingana na mfuko na chaguo lake.

Mgahawa karibu na Ubungo, Tanzania
accommodation in Ubungo, Dar es salaam, Tanzania

CHUMBA CHA MIKUTANO
Hotel ina chumba cha kisasa cha mikutano au sherehe ndogo chenye uwezo wa kukaa watu mpaka 60(mkao wa mikutano). Chumba cha mikutano kina vifaa vya kufundishia na intanet.

VYUMBA VYA WAGENI
Tunatoa huduma nzuri ya malazi ya vyumba vizuri vya wageni katika mazingira ya kirafiki na utulivu. Hii inajumuisha vyumba vinavyojitegemea kwa maji moto na baridi, TV, DVD, kitanda cha kisasa, simu na intanet. Ipo sehemu ya kutosha ya kuegesha magari na yenye ulinzi.

MGAHAWA NA BAA
Tunatoa huduma ya kifungua kinywa, vyakula vya kimataifa na asili mchana na usiku kwenye mgahawa na baa yetu. Vinywaji na vitafunwa vipo katika hoteli yetu. Bei zetu kwa ajili ya malazi pamoja na chai ya asubuhi na chumba cha mikutano ni rahisi ambazo hata watu wa kipato cha chini wakulipa.
Wasiliana na mapokezi au tovuti yetu kujua bei kwa wakati huu.

 
Back to content | Back to main menu